Steve Nyerere, Marehemu Mashaka (katikati) na Vicent Kigosi Ray.
Akizungumza www.eatv.tv Vincent Kigosi amesema ameguswa na msiba huo kutokana historia yake na muigizaji huyo katika kikundi cha Kaole Sanaa Group kupitia maigizo yaliyokuwa yakirushwa kituo cha ITV.
Ray Kigosi amesema "Mashaka ni msanii mkubwa na msiba wake ni mkubwa sana kazi ya mungu haina makosa, ameacha pigo kwenye tasnia ya filamu na maigizo, maana ni mara chache sana kuwa na waigizaji kama wale."
"Wiki tatu zilizopita nilikutana nae kariakoo na nilimwambia kuna project kubwa inakuja nataka kukushirikisha, yaani kikubwa alikuwa mtu mpole sana na mcheshi", amesema Ray Kigosi.
Kwa upande wake Steve Nyerere akizungumza na www.eatv.tv amesema "cha muhimu nilichotaarifiwa watazika kesho, hakuna mtu ambaye hataweza kushiriki maana ni msiba wa msanii mkubwa kwa hiyo wasanii wote tutajitokeza kwa wingi kumzika ndugu yetu Mashaka".
Mapema leo hii kulisambaa taarifa juu ya kifo cha msanii huyo wa zamani wa maigizo ambaye anafahamika kama Ramadhani Mrisho Ditopile (Mashaka), ambapo alifariki dunia katika hospitali ya amana jijini Dar es salaam.




