Jumanne , 20th Feb , 2024

Kundi la Ramadhani Brothers kutokea Tanzania, limeandika historia ya kuwa Watanzania wa kwanza kushinda mashindano makubwa ya kusaka vipaji American Got Talents: Fantasy League.

Picha ya Ramadhani Brothers

Kundi hilo linaloundwa na ndugu wawili (Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu) wametangazwa washindi kwa umahiri wao katika sarakasi (Acrobatics) usiku wa jana Jumatatu na kuondoka na kibunda cha zaidi ya Tsh Milioni 600.

“Hatimaye safari yetu imefikia hapa, tuna furaha kuwa washindi wa AGT Fantasy League duniani, asante kwa mashabiki wote na washiriki wenzetu” - wameandika Ramadhani Brothers baada ya ushindi huo.