Jumatano , 1st Dec , 2021

Raia wameanzisha 'petition' mtandaoni kwa vyombo vya habari kuacha kufanya mahojiano na Will Smith na mkewe Jada Smith baada ya kuchoka kusikia story za ndoa yao.

Will Smith na Jada Smith

Will na Jada tangu waachane wamezunguka katika vyombo vya habari kutoa siri zao za ndani, na sasa mashabiki hawataki kusikia tena story zao na kuanzisha petition ambayo ilianza kwa kuhitaji sign 500 na baadae ikaongezwa mpaka sign 1500 kuwataka waandishi wa habari waache kuwafanyia mahojiano, na mpaka sasa zaidi ya raia 1200 wamesha sign.