Ijumaa , 17th Oct , 2014

Msanii wa muziki Rabbit kutoka Kenya, hatimaye ameweka wazi mtayarishaji muziki ambaye atafanya naye kazi kutoka hapa Tanzania kuwa ni Nisher, na hii itakuwa ni kwa video ya rekodi yake inayokwenda kwa jina Najipendelea.

Rabbit

Rabbit ameweka wazi kuwa, ameunganishwa na mtayarishaji video huyu na wasanii ambao pia ni marafiki zake wakubwa, Joh Makini pamoja na G Nako ambao ndio waliofanya naye kolabo katika ngoma ya Najipendelea.

Rabbit amesema kuwa, kwa sasa mipango inawekwa sawa kutokana na ratiba kubana, ambapo Director anaweka baadhi ya mambo sawa kabla ya kazi kuanza, na hivi ndivyo alivyosema.