
msanii wa muziki wa Uganda Phina Mugerwa
Phina amesema kuwa, anaumizwa sana kumuona Ken akiwa anatumia pesa vibaya huku akisahau matunzo ya mtoto wake, na mbaya zaidi wakati mwingine yeye pamoja na mwanae wakishuhudia anasa anazofanya na mwanamke mwingine kupitia Televisheni na Magazeti.
Phina ameongeza kuwa, amekuwa akimruhusu mwanae Kendton kwenda kumsalimu baba yake lakini hatafanya hivyo tena kutokana na kugundua kuwa Ken akishirikiana na Cindy hawajaweza kuwa mfano mzuri mbele ya mtoto huyu.
