Alhamisi , 20th Nov , 2014

Msanii wa muziki Peter Msechu, amejitapa kuwa licha ya umaarufu wake yeye amekuwa siku zote akiishi maisha ya kawaida ya kistaa, tofauti na mastaa wengi hapa Bongo ambao huigiza kuishi maisha ya kiwango cha juu.

msanii wa miondoko ya bongofleva Peter Msechu

Kwa mujibu wa msanii huyu, katika wasani wote waliopo hapa nchini, asilimia moja pekee ndiyo wanaoishi maisha ya kistaa kwa uhalisia, na wengine wote wanajikuta katika mazingira ya kuigiza ili kuwafurahisha watu wengine, kitu ambacho kinaweka maisha yao katika hatari.