Jumatano , 18th Mar , 2015

Msanii wa muziki Peter Msechu ametangaza kuwa, mwaka huu kwa upande wa sanaa yake ya muziki utakuwa ni wa tofauti sana, akiweka wazi mpango wa kuachia rekodi nyingine mwishoni mwa mwezi huu.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Peter Msechu

Msanii huyu pia akatangaza tena rasmi kuwa endapo rekodi hiyo haitafanya vizuri, basi na yeye ataacha muziki.

Msechu ambaye alikwishatoa kauli kama hii kabla ya kuachia rekodi yake inayokwenda kwa jina 'Nyota', amesema kuwa kazi hiyo baada ya kutoka ndipo binafsi alipoanza kuona matunda ya muziki, akiahidi kuja na rekodi nyingine kubwa zaidi hivi karibuni.

Inafahamika kuwa pia leo ni Birthday ya staa huyu mkali wa Bongofleva, na eNewz tunamtakia furaha na mafanikio tele. (Happy Birthday Peter Msechu).