Jumatano , 13th Oct , 2021

Unaweza kusema ni kama mahaba ya Rapper Billnass na mwimbaji Nandy yamezaliwa upya baada ya kufunga safari mpaka huko Dubai ambako wapo mapumzikoni na kufurahia maisha.

Wapenzi hao wa muda mrefu wameamua kwenda Dubai moja ya miji ya starehe Duniani na kutembelea maeneo mbalimbali kama Jangwani na kula bata licha ya kuwa hivi sasa wamebadilisha mtindo wao wa maisha kwa kuto weka hadharani mara kwa mara mahusiano yao.