Jumatatu , 20th Oct , 2014

Nuh Mziwanda a.k.a Babby wa Shilole, amesema kuwa kuzama katika penzi la bibie huyu na kuingia katika maisha yake kumemfundisha kitu kikubwa kabisa na kila siku anaendelea kujifunza namna ya kuishi katika familia akiwa kama baba katika umri mdogo.

Shilole na Nuh Mziwanda

Mkali huyu ambaye anashine na Ngoma ambayo pia ina bonge moja ya chupa, Msondongoma, amesema kuwa katika hatua ya mwanzo maisha haya mapya ndani ya familia ya shilole, yalikuwa yanampatia changamoto lakini sasa amengundua kuwa hili ni darasa poa kabisa la maisha yake ya baadae ya ubaba.