Jumatano , 28th Feb , 2024

Mwanamuziki wa Nigeria Adekunle Gold amepaza sauti mbele ya umati wa mashabiki wa muziki wake katika moja ya onesho jijini Manchester, Uingereza na kuwatia moyo wahanga wote wanaosumbuliwa na changamoto ya ugonjwa wa seli mundu kama yeye na kuwaambia wasivunjike moyo na kujiona wanyonge.

 

'Nilizaliwa na selimundu, nimeishi nayo maisha yangu yote. Kama mimi nimeweza hata ninyi mnaweza. Nimepambana nayo hadi kuwa staa, nafanya shows mahali popote duniani hata isiwavunje moyo' amesema Adekunle.

Mnano Julai 2022, kwa mara ya kwanza Adenkule alifichua kuwa amekuwa akiishi na ugonjwa wa selimundu tangu kuzaliwa kwake na namna ambavyo alipitia kipindi kigumu katika kupambana na hali hiyo.

Kwa mujibu wa wataalamu Seli Mundu (Sickle Cell) ni ugonjwa ambao hushambulia seli nyekundu za damu pamoja na haemoglobin ambapo huhusisha mtu kuishiwa damu.