Jumatatu , 10th Mei , 2021

Fundi wa magari Uchebe ameshea stori kwamba aliwahi kuwa katika dini ya Uikristo lakini akaamua kubadili dini hiyo na kuhamia kwenye Uislam.

Picha ya Uchebe

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Uchebe amesema hiyo ni historia ndefu ila watu wafahamu kwamba amehamia kwenye Uislam zaidi ya miaka 8 iliyopita na ana imani atafanikiwa katika dini hiyo.

"Ni historia ndefu sana lakini mimi nimesilimu karibia miaka 8 na zaidi iliyopita, wajue tu mimi nilikuwa mkristo nikasilimu kuwa muislam,  mpaka leo ni muislam na kwa uwezo wa Allah nitaenda kufanikiwa nikiwa muislam, kipindi hicho nilikuwa kijana wa kawaida tu ambaye napambana na maisha yangu" amesema Uchebe