Ijumaa , 23rd Feb , 2024

Hawa ni baadhi ya watu maarufu duniani ambao hawapo katika mitandao ya kijamii ikiwemo Instgram na X zamani (Twitter) licha ya umaarufu na nguvu kubwa ya ushawishi waliyonayo hasa katika sanaa. Wapo waliowahi kuingia na kutoka kwasababu zao binafsi, na wengine hawakurudi tena mtandaoni

Jay-Z; licha ya kuwa mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop wenye ushawishi zaidi duniani huwezi kumpata Instagram wala X. Japo amewahi kujaribu kufungua akaunti Instagram na kuifuta baada ya saa chache tu, mfano Nov 2021 pia kuna akaunti iliyo Verified kwa jina la Mr.Carter kwenye X ambayo haimilikiwi na Jay Z.  Amezaliwa mwaka 1969.
-
Eddy Murphy; Mchekeshaji na mwigizaji maarufu duniani kutoka Marekani; hayupo katika mtandao wowote kuanzia Facebook, X wala Instagram. Amezaliwa mwaka 1961.
-
Jennifer Lawrence; Mwigizaji maarufu wa Marekani amabye hatumii mtandao wowote wa kijamii, hayupo Instagram wala X. Jennifer amezaliwa mwaka 1990.
-
Merghan Markle ambaye ni mke wa Mwanamfalme (Prince Harry) wa Uingereza, aliolewa mwaka 2018 na hapo kabla alikuwa Mwigizaji na Mhamasishaji, hana akaunti yoyote ya mtandao wa kijamii. Merghan amezaliwa mwaka 1981.
-
Tom Holland; Mwigizaji maarufu kutokea Uingereza, alitangaza kuchukua break ya kutokutumia mitandao ya kijamii tangu mwaka 2022 ili kukabiliana na changamoto ya afya ya akili iliyokuwa ikimkabili. Tom amezaliwa mwaka 1996.
-
Brad Pitt; Mwigizaji maarufu na Mtayarishaji mkongwe wa filamu nchini Marekani, hatumii mtandao wowote wa kijamii. Amezaliwa mwaka 1963.
-
Emma Stone; Mwigizaji maarufu wa kike na Mtayarishaji wa filamu nchini Marekani, hayupo katika mtandao wowote. Amezaliwa mwaka 1988.
-
Emily Blunt; licha ya mumewe John Krasinski kuwa katika mtandao wa Instagram, Emily Blunt ambaye ni mwigizaji maarufu kutokea Uingereza, yeye hatumii mtandao wowote wa kijamii na mara kadhaa amewahi kunukuliwa akisema anaishi kwa furaha. Emily amezaliwa mwaka 1983.
-
Tutajie mastaa wa hapa Bongo unaowafahamu hawapo katika mitandao yoyote ya kijamii.