
Msanii wa muziki wa bongofleva M2 The P akiwa na marehemu Albert Ngwair
Kwa upande mwingine, Noorah ambaye walikuwa wakiunda kundi la Chamber Squad na Mangwair amesema kuwa, akikumbuka wakati wote waliokuwa pamoja, toka Mazengo Dodoma, mpaka Kijitonyama Dar es Salaam, majibu pekee anayopata ni hakuna yeyote yule anayeweza kuwa kama Ngwair.
Vilevile M2theP, ambaye alikuwa karibu na marehemu siku anapoteza maisha tarehe kama ya leo huko Afrika Kusini, kuhusiana na kumbukumbu ya tukio hilo amesema matamasha yatafanyika Dar na Morogoro kumuenzi star huyo.
eNewz tunaiombea roho ya Marehemu mapumziko mema mahala pema peponi, Aamin.
