Jumanne , 4th Mei , 2021

 Wimbo wa Nay wa mitego “Mama” wakwama BASATA kutokana na kukosa vigezo baada ya kukaguliwa.

Msanii Nay wa Mitego

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kupitia kaimu katibu mtendaji Matiko Mniko alitangaza kuwa kuanzia tarehe 1 mei wataanza kutumia kanunu ya kuzipitia nyimbo mpya za wasanii wote Tanzania kabla ya  kupelekwa kwenye vituo vya Redio na Runinga.

Jamatatu mkali huyo wa hip hop alikuwa aachie kazi yake mpya lakini hakufanya hivyo baada ya wimbo huo kukwama kutokana na marekebisho ambayo ameamriwa na baraza kuyafanya.