Nay aijibu BASATA "Siwezi badili chochote"

Jumanne , 4th Mei , 2021

Rais wa kitaa Nay wa Mitego amenyoosha maelezo kufuatia taarifa za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuukataa wimbo wake na kumtaka aurekebishe kwa sababu una ukakasi hivyo haufai kwenda hewani.

Msanii Nay wa Mitego

Akizungumzia hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio Nay wa Mitego ameeleza kuwa

"Wimbo wameukataa wanasema una ukakasi nifanye marekebisho, sasa mimi tayari nishafanya video na kila kitu, nilisikiliza kitu ambacho wametaka nirekebishe au nitoe kwenye wimbo ndio content yenyewe, nikitoa itakuwa sio wimbo tena ni Gospel"

"Nia yangu ni kuhamasisha wakina mama kwamba wanaweza kufanya kitu ndio kikubwa nilichokizungumza kwenye wimbo, sikutegemea utaonekana una tatizo, baada ya kuja jibu hilo nikasema siwezi kubadilisha chochote bora niachane nao japo inauma na nimepata hasara"

Aidha msanii huyo ameendelea kusema "Natamani Mama atakuja kusikia na ataona kabisa watu kiasi gani wanakurupuka, waliokaribu na Mama naomba wamwambie tu nampenda kuliko mtu yeyote anavyompenda, namjali na nina kitu kwa ajili yake lakini watu hawataki kusikia".

Zaidi mtazame hapa akizungumzia hilo.