
Navio katika kazi hii mpya amemshirikisha msanii Stephanie Ming, na kazi hii imerekodiwa huko Atlanta nchini Marekani, ambapo pia kabla ya kukamilika imepitia katika mikono ya Kid Class ambaye naye pia ana rekodi kubwa ya kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa kimataifa.
Rekodi hii mpya kutoka kwa Navio, inakuja kama hatua nyingine kubwa ya rapa huyu kuiweka Uganda katika ramani ya muziki ya kimataifa sambamba na kusimama pia yeye kama Navio, katika nafasi ya juu kabisa akiwa kama rapa kutoka Afrika Mashariki.