Alhamisi , 24th Nov , 2016

Msanii Navio ambaye ni rapa kutoka nchini Uganda, ameelezea furaha kuwa msanii pekee wa kiume kutoka Uganda kuwa 'nominated' kwenye Tuzo za EATV (EATV AWARDS).

Navio

 

Akizungumza na EATV Navio amesema ni furaha kwake kuwa miongoni mwa washiriki wa tuzo hizo, na pia kushindania kipengele kimoja na wanamuziki wakubwa kwa Afrika Mashariki akiwemo Lady Jayedee, Joh Makini na Alikiba.

"I'm feeling good, its nice to be in the same category with my boys, a nice and hard category, its nice being in a category where others are doing such amazing job, i feel like i'm around my field, i'm glad to have glamorous woman  as well, Jaydee has always done an amazing job, and then my boys Alikiba, me and Joh Makini is East African Hip Hop" . Amesema Navio akimaanisha ( Najisikia vizuri, ni vizuri kuwa kwenye kipengele kimoja na vijana wangu, ni kipengele kizuri na kigumu, ni vizuri kuwa kwenye kipengele kimoja ambacho wengine wanafanya kazi za kushangaza, najihisi kama nipo kwenye uwanja wangu, nina furaha pia kuwa na mwanamke mwenye uwezo mkubwa, Jaydee anafanya kazi nzuri, Alikiba mimi na Joh Makini.", alisema Navio.

Tags: