Picha ya msanii Nandy
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Nandy amesema yeye ni mtu wa kwenda kanisani siku zote ila aliyoyafanya siku ya kuukaribisha mwaka mpya yalikuwa ni maombi maalum.
"Mimi ni mtu ambaye nashiriki sana ibada, napenda kusali kwa Mwamposa maana ndiyo Baba yangu wa kiroho, nikisema nimeokoka watu wanaweza wakatafsiri tofauti kwa sababu wanaweza wakahoji, nimeokoka halafu nafanya muziki ila ni mtumishi wa Mungu vizuri tu, natenda yale mema" ameeleza Nandy.
Aidha Nandy ameendelea kusema "Hakuna kitu nafanya bila ya kumshirikisha Mungu hiyo nayo ni kuokoka pia, kuna vitu vingi najiepusha navyo kama binadamu kutokuvifanya, kama havimpendezi mwenzangu mimi nisimfanyie au visivyonipendeza nisifanye huko ni kuokoka pia ila ni muumini mzuri tu wa dini" ameongeza.





