Jumanne , 15th Dec , 2015

Msanii Mzungu Kichaa ameamua kufanya mkakati wa kutambulisha bendi na timu yake nzima akizunguka na gari katika kona za mitaa ya Dar es Salaam, mchakato wa tofauti ambao pia umeenda sambamba na kupiga picha za kazi hiyo mpya.

msanii wa miondoko ya bongofleva Mzungu Kichaa

Mzungu Kichaa ambaye amekuja na wazo hilo tofauti kutokana na wigo mkubwa wa ujuzi alio nao kitaifa na kimataifa, baada ya kukamilisha mchakato huo anatarajia kushiriki na mashabiki kwa kutoa kazi hiyo kama video, ikisimama kwa jina Relax Your Mind kama anavyoeleza mwenyewe hapa.