Jumatatu , 13th Jul , 2015

Muigizaji mkongwe wa vichekesho nchini Kenya, Benson Wanjau maarufu kama mzee Ojwang amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya taifa ya Kenyatta alipokuwa amelazwa.

Muigizaji mkongwe wa vichekesho nchini Kenya marehemu Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang

Mzee Ojwanga alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na maradhi ya Nimonia.

Muigizaji huyo ambaye alikuwa ni kinara katika vipindi vya Vitimbi, Vioja Mahakamanii, Vituko na Kinyonga pamoja na nyinginezo alikuwa hajaonekana kwenye televisheni kwa muda mrefu.