
Kwa mujibu wa msemaji wa kundi hilo la Radio &Weasel, msanii Radio amefariki leo majira ya saa 12 asubuhi na watazungumza na waandishi wa habari muda si mrefu kuhusu taratibu za msiba na mazishi
Radio amefariki leo ikiwa ni kama wiki mbili zipite tangu alipofikishwa hospitali baada ya kupata majeraha kutokana na kupigwa vibaya sehemu ya kichwani , akitokea kwenye hoteli moja huko Entebe nchini Uganda.
Pamoja na hayo taarifa kutoka uongozi wa Hospitali alikolazwa Msanii Radio umekiri kupokea na kushukuru Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa kuchangia kiasi cha fedha za Uganda Milioni 30 kwa ajili ya matibabu.
Msanii radio amefariki akiwa na umri wa miaka 33.
Msanii radio pamoja na Weasel kwa pamoja waliunda kundi la Goodlyfe Crew ambapo ndani ya muungano huo walishirikiana kutoa ngoma kali kama Gutamiza, mama, Lola na huku kwa Tanzania wakiwa wameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo Vanessa Mdee, Lady JayDee, huku Dogo Janja akiwa amefanya My Life remix