Alhamisi , 2nd Nov , 2023

Vyanzo mbalimbali vya habari Kenya na wasanii wa nchini humo wameshea taarifa ya kifo cha Mwanamuziki mkongwe Ally B ambaye amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi wakati anapatiwa matibabu Hospitali ya Makadara Mombasa.

Picha ya aliyekuwa msanii Ally B

Taarifa zinasema marehemu Ally B alianza kujisikia vibaya na kukimbizwa Hospitali ambapo umauti ulimkuta. Msanii huyo alitamba na nyimbo za Maria na Bembea.