Ijumaa , 14th Mei , 2021

Mr Seed anavunja ukimya siku chache baada ya mrembo mmoja (side chick) huko Kenya kutangaza kuwa ana ujamzito na mwimbaji huyo maarufu wa Injili.

Msanii Mr Seed

Wakati yupo mapumziko na mke wake “Nimoh Gachuiri” huko pwani ya Kenya alitumia muda huo kukanusha taarifa zilizokuwa zikiendelea kusambaa juu ya mwanamke aliyekuwa akimtuhumu kuwa alikataa mimba yake na kumlazimisha aitoe.

Seed amesema kuwa siku zote ni mwenye furaha bila kujali mambo yanayotokea maishani mwake, licha ya kashfa za ngono kuendelea kumuandama za kutoka kimapenzi na warembo tofauti tofauti.