Jumanne , 19th Jan , 2016

Richard Sebadduka (aka Mr. Flava ) toka Uganda mwenye uzoefu wa zaidi ya mika 10 katika sekta ya masuala ya kumsaka mrembo anayewakilisha Uganda ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taifa wa mashindano ya Miss Umoja wa Mataifa kwa Uganda

( Miss United Nations for Uganda).

Pia Mr. Flava ameteuliwa rasmi kuwa Mratibu wa mashindano ya Miss Umoja wa Mataifa kwa bara la Afrika (official Miss United Nations Cordinator for African continent).

Uteuzi huo umetolewa na Rais wa UNP na mwanzilishi wa mashindano hayo anayeishi Jamaica Mh Leon Williams.

Habari zaidi kwa ajili ya mipango ya Miss Umoja wa Mataifa Uganda tukio 2016 zinakuja.