Picha ya Obama na mkewe Michelle Obama, kulia ni mwanamuziki Beyonce
Kupitia page ya mtandao wake wa X Michelle Obama ameandika
“Beyonce wewe ni mvunja rekodi na muweka historia. Ukiwa na Cowboy Carter, umebadilisha game kwa mara nyingine tena kwa kusaidia kufafanua upya aina ya muziki na kubadilisha utamaduni wetu. Ninajivunia wewe”
“Album hii inatukumbusha kuwa sote tuna uwezo. Kuna nguvu katika historia yetu, furaha yetu, kura zetu na kila mmoja wetu anaweza kutumia vipawa na talanta zetu ili kufanya sauti zetu zisikike kuhusu masuala muhimu sana kwetu”.
Cowboy Carter ni Album ya 8 studio ya Beyonce ambayo imetoka Machi 29, 2024 ikiwa na mikwaju 27.