Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Wate r amesema wakati anaanza muziki alianza kwa kurap na kuimba, lakini alichoshwa na changamoto alizokutana nazo, alipokwenda studio kutaka kurekodi.
“Huu muziki nilianza kwa kuimba, nilikuwa napenda kurap, tulikuwa tunapiga showMwamba, lazima utengeneze demo yako kwenye tape, wakati ule mi nachana lakini nina idea ya kuimba, nilikuwa tu nataka kuwa msaniii, nikitoka nje wasanii wanalalakmika, ndo nikaamua na mimi niwe na studio yangu”, alisema Man Water.
Pia Man Water amesema hata hivyo wakati wa kuhangaika kutoka, hakuwahi kukutana na Mika Mwamba, kutokana na jinsi mfumo wa kipindi hiko ulivyokuwa, na badala yake alikuja kuonana na Mika Mwamba hivi karibuni, akiwa producer.



