Ijumaa , 28th Mei , 2021

Leo ni miaka 8 tangu alipofariki dunia mfalme wa freestyle kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Albert Keneth Mangwair ‘Mangwair’, kilichotokea huko Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Picha marehemu Mangwair

Mei 28, ndiyo huwa kumbukizi ya kifo chake ambacho kilichotokea ghafla mwaka 2013, na anakumbukwa kutokana na uwezo wake mkubwa aliowahi kuonesha kwenye kazi zake mbalimbali  na aina yake ya kipekee ya kuchana.

Mwana Chemba Squard huyo alifanikiwa kutamba na Hits kama ‘Weekend, Mikasi na Ghetto langu’ huku mwaka 2005 aliibuka mshindi wa tuzo za KTMA kama mwana Hip Hop Bora.