
Pichani Mbosso,Aslay Na Zuchu
Akipiga story na waandishi siku ya leo Mbosso amesema..
"Ukisema mimi sina mahusiano mazuri na Zuchu au msanii yoyote wa Wcb Wasafi sidhani kama ni kitu sawa mimi ni mmoja wa wasanii ambaye naishi na wasanii wenzangu vizuri na kwenye kila kazi ya wasani wenzangu nawapa kipaumbele''
''Na ndio maana imenipa urahisi zaidi kwenye kazi zangu kuwa kipaumbele kujitoa ndio maana umewaona Zuchu na Diamond wamkuja kuniona na tayari nimeshatoka Wcb Wasafi kwahiyo kama tungekuwa hatupo sawa wasingekuja nadhani hayo ni maneno tu na kila mtu anaongea lake''Amesema Mbosso
Kuhusu Msanii mwenzie Aslay kujiunga Label ya Wcb Wasafi msanii Mbosso amesema kuwa...
''Ukipata nafasi yakujiunga Wcb Wasafi maana yake ni neema kubwa kwahiyo mimi napenda kila msanii anayeenda kwenye mafanikio, yani mafanikio ndio yanayotutenga sisi na upambanaji wa umasikini, Hivyo natamani kila mtu afanikiwe na kama Aslay kama amepata ofa nzuri aende'' Amesema Mbosso