Nyota wa muziki wa injili hapa nchini, Emmanuel Mbasha
Mbasha amewataka pia watanzania na mashabiki wake kufahamu kuwa kwa sasa mbali na kujikita kuombea amani, kutokana na kuwa na muda na akili iliyotulia baada ya kufanikiwa kumaliza kesi yake, amewekeza nguvu katika kufanya video na pia kuisukuma albam yake mpya Haribu Mipango ya Shetani.
Mbasha ambaye hakutaka kuongelea masuala binafsi ya familia yake kwa sasa, akionekana mwenye furaha amesema kuwa amani ya nchi, vilevile kazi zake za muziki ndio kitu alichoweka mbele kwa sasa kama anavyoeleza hapa.