Jumatatu , 17th Mar , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Ronald Mayinja ambaye ana sifa kubwa ya kuwa na watoto wengi kutoka kwa mama wapatao 12 ama zaidi, ameamua kusimama imara na kuwawekea watoto wake wote mpango wa kuwa na maisha mazuri.

Mayinja ambaye idadi kamili ya watoto wake bado haijafahamika, amesema kuwa kitendo cha kuwa na idadi hii ya watoto pamoja na mahusiano aliyotengeneza idadi kubwa ya wanawake ambacho kinaonekana si sawa mbele ya jamii, hakimzuii kuanza kusimamia majukumu yake kama baba wa watoto.

Tayari mke wa msanii huyu, Aisha Mayinja ameonyesha kumuunga mkono msanii huyu na kusema kuwa, anakaribisha watoto wote ambao msanii huyu amewapata nje ya mahusiano yao, na yupo tayari kushirikiana nao katika kuyajenga maisha.