Jumatano , 15th Jul , 2015

Baraza la Seneti limesema serikali ya Kenya ilimtelekeza muigizaji mkongwe na maarufu Mzee Ojwang' aliyechangia katika kuhamasisha umoja miongoni mwa wakenya, akifariki dunia akiwa masikini

aliyewahi kuwa mchekeshaji nyota wa Kenya marehemu Mzee Ojwang

Wakijadili muswada wa kutambua watu waliofanikiwa kwa mchango wao kwa Taifa, Maseneta wamesema ilikuwa ni kosa kumuacha Mzee Ojwang' kufariki dunia bila kutambuliwa mchango wake na Ikulu.

Maseneta hao wameikosoa serikali ya Kenya kwa kungojea mashujaa wa taifa wafe kwanza ndipo waanze kuwapongeza kwa mambo makubwa waliyolifanyia taifa.