Katika kazi hiyo ambayo ilikuwa video yake ya mwisho aliposainishwa katika lebo hiyo inajulikana kwa jina ‘Give it to me’ akimshirikisha J Martins ambayo ilikuwa itoke rasmi siku ya wapendanao yaani Valentine Day, siku ambayo Goldie alifariki dunia baada ya kuzimia hafla akiwa nyumbani kwao Jijini Lagos.
Jumatatu , 17th Feb , 2014
Msanii wa kike wa Nigeria marehemu Goldie Harvey ana kila sababu ya kukumbukwa haswa katika fani yake ya muziki ambapo habari zilizopo ni kuwa Goldie aliacha moja ya kazi zake ambazo zilikuwa zimehifadhiwa chini ya lebo yake iitwayo Kenis Music.