Jumapili , 2nd Jun , 2024

Kweli umri ni namba tu kwenye Mapenzi! Unaambiwa Mama mzazi wa Kim Kardashian na binti zake wengine Kris Jenner amempita miaka 25 mpenzi wake Corey Gamble.

Picha ya Kris Jenner na mpenzi wake

Wawili hao wametimiza miaka 10 ya mahusiano yao wakati Kris Jenner ana miaka 68 na Corey miaka 43 sawa na umri wa Kim Kardashian.

Kuhusu kupishana miaka hiyo 25 kwenye mahusiano yao, Kris Jenner amesema 

“Nilikuwa nikimwambia Corey nilipoanza kuchumbiana naye kwamba kwanini unataka kuchumbiana na mtu ambaye ni mkubwa? Akanifundisha umri ni namba tu, hata kama mkubwa”.

“Siwezi kuelezea Chemistry ya mtu au kwa nini watu hupenda lakini imekuwa ya kushangaza karibu miaka 10, na tuna wakati mzuri”.

Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema Corey Gamble amejipatia zake mshangazi Kris Jenner.