Jumatatu , 10th Mei , 2021

Baadhi ya wasanii na watu maarufu wengi duniani wamekuwa na 'style' ya kufunga mbwa wadogo aina ya 'Puppy' ambao huwafanya kuwa wanyama rafiki wawapo nyumbani kwao au hata kwenye mitoko yao.

Msanii Malaika na mbwa wa aina ya Puppy

Sasa msanii wa muziki Malaika amenyoosha maelezo kuhusu matumizi ya mbwa hao ambaye hata yeye anaishi nae nyumbani kwake Kigambono Dar es Salaam.

"Kigamboni ninao majirani sipati Upweke nyumbani kwa sababu kuna wageni wanakuja, matumizi ya vile vi-puppy (Mbwa) huwa vinakupa company, unamtoa nje na yeye ku-enjoy" amesema Malaika

Staa wa filamu Wema Sepetu aliwahi kuweka dau la Tsh Milioni 1 mpaka 2 kwa mbwa wake wa aina hiyo aitwaye Manunu alivyopotea, hata Aliyekuwa Rais wa Marekani awamu ya 44 Barack Obama naye anaomboleza kifo cha mbwa wake aitwaye Bo ambaye amekufa kwa Ugonjwa wa Kansa.