Ijumaa , 4th Sep , 2015

Makundi 10 ambayo yamefanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Dance 100 2015, leo hii yameweza kupatiwa semina elekezi sambamba na kuchagua miziki ambayo watatumia katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo tarehe 19 mwezi huu.

Moja ya madansa kutoka kundi la Cute Babies akionyesha CD ya nyimbo waliyojichagulia

Kutokana na utaratibu wa hatua waliyofikia, makundi hayo ambayo ni Majokery, Wazawa Crew, The Best, Cute Babies, Best Boys Kaka Zao, The Winners, Team ya Shamba, The WD, Team Makorokocho na Quality Boys, yatalazimika kupanda jukwaani kwa mizunguko miwili, mmoja ukihusisha kudansi muziki waliojichagulia leo, na mwingine ukihusisha muziki waliouandaa wenyewe.

Sambamba na uchaguzi huo, madansa hawa pia walipata mawaidha kutoka kwa uongozi na waratibu, ili kuivuka hatua hiyo kwa taratibu zilizowekwa.

Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea fainali ya mashindano haya makubwa, kila kundi likinuia kuchukua zawadi nono ya fedha taslim shilingi milioni 5, kumbuka Burudani hii yote inaletwa kwako na EATV na East Africa Radio, kwa udhamini mkubwa Vodacom Tanzania na kinywaji cha Coca Cola.