Jumamosi , 24th Sep , 2016

Shindano la Dance100% 2016 limemalizika leo katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam ambapo kundi la Makorokocho limeibuka na ubingwa na kujipatia kitita cha milioni 7, Kombe la Dance100% pamoja na cheti maalum.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka Vodacom Jacquiline Materu akikabidhi mfano wa hundi ya milioni 7 kwa kusni la Timu Makorokocho

Ushindi wa Team Makorokocho umekuja baada ya makundi yote 6 kucheza raundi ambapo raundi ya kwanza Mega Mix waliyoandaliwa, na ilichezwa na makundi yote ikiwa na jumla ya alama 60% huku raundi ya pili ikiwa na alama 40% ambapo kila kundi lilijichagulia wimbo wake wa kucheza. .

Baada ya kazi ya raundi zote mbili kazi ya majaji ilikamilishwa na shughuli ya kumuisha matokeo na hatimaye kundi la Team Makorokochokuibuka na ushindi mwaka huu kutokana na uwezo waliouonesha katika raundi zote mbili na kuyapiku makundi yote.

Akizungumza baada ya kuibuka washindi wa shindano hilo Hamadi Abasi amesema umoja na mshikamano katika kundi lao ndicho chanzo kikuu cha wao kuweza kuibuka na ushindi wa shindano hilo.

“Sisi kutokana na umoja wetu tumekuwa zaidi ya ndugu ndiyo maana tumeweza kuwa wamoja katika mazoezi na kujituma na kuangalia wenzetu wana upungufu gani tukaufanyia kazi na hatimaye tukatangazwa washindi” Amesema Hamadi.

Hamadi ameongeza kuwa ushindi wao hauna ubishi wowote kwa kuwa ukiondoa majaji pia hadhira ambayo imeshiriki kutizama shindano wameona kazi ambayo wameoinesha .

Matokeo yote kwa makundi yote 6 yaliyoshiriki fainali ni kama ifuatavyo kwa mpangilio wa namba.

Timu Makorokocho
J Combat
D.D.I Crew
Clever Boys
Wazawa Crew na kundi la mwisho ni B.B.K Boys

Baadhi ya mashabiki ambao wameongea na EATV wamesema kundi hilo linastahili ushindi huo kutokana na namna ambavyo kuanzia mwanzo wa shindano hilo wameonesha dhamira ya kutaka ushindi kwa kuwa wabunifu kila siku wanaposhiriki shindano.

Shindano la Dance100% ambalo limefikia tamati leo litaoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni chini ya udhamini wa Vodacom pamoja na Coca – Cola.

Tags: