Alhamisi , 26th Nov , 2015

Kutoka kundi mahiri la Makomandoo, msanii wa muziki Muki ameeleza kuwa kutokana na kubadilika na kukua kwa kasi kwa soko la muziki, ushindani na mkakati wao wa kufanya kazi umebadilika kwa kiasi kikubwa tokea waanze kutambulika katika gemu.

msanii wa muziki Muki Kutoka kundi mahiri la Makomandoo

Kutambulika huko na kubadilika kwa soko la muziki huo ni baada ya kujigundua kuwa wanashindana na nchi nyingine na si wasanii wa hapa ndani tena.

Muki kwa niaba ya Makomandoo ameeleza kuwa, katika kufahamu mbio za muziki zimekuwa kubwa, wakishindana na nchi kama Nigeria, Afrika Kusini na kwingineko, hiyo ndiyo tafsiri pekee ya kuachia kazi mbili ndani ya kipindi kifupi sana, pia wakiwa katika mpango wa kuzindua rasmi video katika show ya Friday Night Live.