
Picha Producer P-Funk Majani na Rapcha
Kupitia instagram Majani ameonesha kuvutiwa na mapokezi ya wimbo huo ‘Lissa’ ambao una siku chache tu tangu umetoka na kufanikiwa kushika namba 2 kwenye trending for music, ikiwa umetazamwa na kusikilizwa na watu zaidi ya laki 3 huko YouTube.
“Lissa 2 audio yake ipo tayari, ila nina ombi moja, tubaki trending no.1 mpaka Jumapili, na views zifike kuanzia 777,777, Muziki wa Hip Hop upewe heshima yake unayostahili, Jumatatu nashika kamera, nawapa Movie la hatari kabisa”- ameandika Majani.