
Msanii Hussein Machozi
"Nimeamua kuweka style hii ya nywele niliyoiita kuchi, kuchi ni nyoya la kuku ambaye akipigana huwa anahakikisha anashinda hata kama akifa lakini kikubwa ashinde, na mimi nimeliweka hili nyoya nikimaanisha sichoki mpaka nishinde" amesema Hussein Machozi
Msanii huyo kwa sasa amerudi nchini Tanzania baada ya miaka 7 ambayo alikuwa anaishi nchini Italy ambapo akiwa huko ameweza kupata mke na mtoto mmoja.
Pia ameongeza kusema wakati anaishi Italy alikuwa anafanya kazi ya uwalimu wa kufundisha watu kuteleza kwenye barafu japo amekutana na changamoto za kubaguliwa na baadhi ya raia wa Italy.