Msanii wa BongoFleva Lady Jay Dee
Maajabu ya Album hiyo kuitwa jina la 20 ni kutokana na yeye kukaa kwenye game kwa miaka 20 tangu mwaka 2000, pia ndani ya Album hiyo kutakuwa na jumla ya nyimbo 20.
Akifafanua hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Lady Jay Dee ameeleza kuwa "Album yangu ya nane itaitwa 20, hii ni kutokana na kwamba itatoka mwaka huu 2020 ambapo naadhimisha miaka 20 kwenye kiwanda cha muziki, pia Album hii itakua na jumla ya nyimbo 20".

