
Mzungu Kichaa amefunguka hayo alipokua akihojiwa katika kipindi cha Muziki wa Bongo cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha EATV.
“Muziki wa Bongofleva unakua na unafanya vizuri kimataifa lakini wanamuziki watakapofanya muziki huu live itasaidia kuupeleka mbali zaidi muziki wa Bongofleva katika soko la kimataifa,” alisema mwanamuziki huyo huku akiwataja wanamuziki kama Ali Kiba, Joh Makini na Fid Q kama wasanii wanaojitahidi ku-perfom Live katika shoo zao.
Aidha, mzungu kichaa ametiririka zaidi kuhusiana na malipo ya shoo huku akitaja moja ya shoo kubwa zilizowahi kumlipa vizuri kuliko shoo zote ni tamasha la Skenderborg, likiwa moja kati ya matamasha makubwa ya muziki nchini Denmark linalohudhuriwa na takribani watu zaidi ya 45,000.
Akigusia kwa ufupi maisha yake binafsi ya mahusiano mwanamuziki huyo amesema ana mtoto mmoja aliyezaa na msichana wa kinyalukolo (Kinyakyusa). Kwa sasa mwanamuziki huyo anatamba na ngoma kali ya “TWAJIACHIA” akiwa amemshirikisha mwanamuziki Malfred, matengenezo ya wimbo huo na kichupa chake yote yamefanyika nchini Ujerumani.