
Wakazi ameyasema hayo alipokuwa akiongea na timu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa kuwepo miongoni mwa wasanii 6 kati ya wasanii zaidi ya elfu kumi, ni ushindi mkubwa kwake.
“Kiukweli mpaka sasa hivi sielewi imekuwa kuwa vipi lakini ndo hivyo namshukuru mwenyezi Mungu kwa sababu nimefanya kazi zangu za muziki na hatimaye baadhi ya watu wanaanza kurecognize, ni kitu cha kujivunia, suala la kuwa nominated tu mi nachukulia tu kama ni ushindi tayari, kwa sababu wasanii wako wengi so kuchaguliwa wasanii sita kati ya ma hip hop artist ambao wanazidi elfu kumi ni kitu cha ushindi tayari kiukweli”, alisema Wakazi
Wakazi amesema pamoja na kuwa miongozi mwa wasanii hao 6 wanaowakilisha nchi zao kwenye tuzo za KORA, bado anahitaji nguvu kubwa kutoka nyumbani kwani bila wao hataweza kushinda tuzo hiyo ambayo italeta heshima kwa Tanzania.
“Bado tunasikilizia information hizo tukiweza kuzipata tu nitaweza kuwasiliana na watu wangu wote na kuona ni jinsi gani wanaweza wakanisaidia kunipigia kura na kuweza kuhakikisha naileta hii tuzo nyumbani, mi naiwakilisha nchi yangu sio wakazi, ushindi wangu utakuwa unatokana na suport ya hapa nyumbani kwa sababu mpaka kufika hapa suport ya other musician, media na mashabiki ndio imesababisha mimi nifike hapa”, alisema Wakazi.
KORA bado haijatoa maelezo jinsi ya kushiriki kwenye tuzo hizo na kuwapigia kura washiriki, na mara taarifa hiyo itakapotolewa Msanii Wakazi ameahidi kuwajulisha mara moja ili mashabiki waweze kumpigia kura.