Kivurande alazwa Hospitali ya Mwananyamala

Jumanne , 8th Jun , 2021

Mkali wa muziki wa kibaokata hapa nchini Kivurande Junior amehamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya hali yake kubadilika wakati alipokuwa amelazwa Hospitali ya Salamani iliyopo Magomeni.

Picha ya Kivurande akiwa Hospitalini

Chanzo cha kulazwa kwa msanii Kivurande inaelezwa kuwa amepata tatizo la kushindwa kuvuta pumzi kwa sababu ya moshi uliomuingia wakati wa jaribio la kuzima moto ulioibuka katika nyumba aliyopanga kama frem ya biashara.

EATV & EA Radio Digital inatoa pole kwa mashabiki wa Kivurande na muziki kwa ujumla pia tutazidi kufuatilia taarifa zote kuhusu maendeleo yake ya Hospitalini.