Jumapili , 14th Jul , 2024

Ni mtazamo wa ‘BIG Joe’ or JK Joseph Kusaga juu ya kuwakutanisha mastaa wa muziki Tanzania Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize kufanya Hit 1 kwa ajili ya kuvusha muziki wa Tanzania barani Africa.

Picha ya Diamond Platnumz, Harmonize na Alikiba

Anaamini kwa nguvu kubwa waliyonayo wasanii hao wakiwekeza kufanya kitu kimoja itainua muziki wa BongoFlava zaidi nje.

“Kikubwa ni kuvunja kambi zisizokuwa na ushirikiano. Nitawaomba kina Alikiba, DiamondPlatnumz na Harmonize tuwe na uwezekano wa kwa nini tusifanye ‘One Hit’ na kuvuka nje ya Africa”. amesema Joseph Kusaga

Comment yako ni ipi kuhusu hilo Alikiba Diamond Platnumz na Harmonize kufanya Hit ya Pamoja?