Jumanne , 13th Feb , 2024

Unaambiwa rapa Kanye West ‘Ye’ amejawa furaha ya mahusiano/ndoa kwa mke wake Bianca Censori na kila siku kwao ni Valentine Day mahaba mwanzo mwisho.

Picha ya Kanye West na Mke wake Bianca Censori

Kanye West amefunguka hilo baada ya mashabiki kuanza kujaji anavyompost mkewe mitandaoni siku za hivi karibuni akiwajibu kwa kuwaambia ataendelea kumpost sababu ndio furaha yake na anafurahishwa na jambo hilo.

“Nampost mke wangu ninavyotaka, inanifurahisha watu wengine hawataki ufurahi wanataka uwafurahishe. Niliamua kujifurahisha na nimefurahishwa na hilo” amesema Kanye West

Lini mara ya mwisho kupostiwa na mpenzi wako mitandaoni?