Kanye aendelea kuteseka na Urais

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Rapper Kanye West ameendelea kukumbwa na jinamizi la kesi, kisa Urais aliokuwa akiutaka mwaka 2020, inaelezwa kuwa kampuni ya SeedX Inc imemfungulia kesi Mahakani kwa kukiuka mkataba wa kazi walioingia mwezi wa 7.

Msanii Kanye West

Kwa mujibu wa taarifa za Mahakama zilizodakwa zinaeleza kuwa kampuni ya SeedX walifanya kazi kwa kipindi cha miezi 3 ya kuandaa taarifa, kuandaa mipango mkakati ya kampeni, kubuni na kuandaa matangazo, kujenga mahusiano na vyombo vya habari na kadhalika pasipo malipo yoyote.

Kampuni ya Lincoln Strategy Group ndio walifanya makubaliano na kampuni ya SeedX Inc kwa niaba ya Kanye mwezi Julai, 2020 ambapo thamani ya shughuli zote za kampeni ilikuwa dola milioni 10 na mpaka sasa dola  milioni 1.5 pekee ndizo zimelipwa.

Kanye West Julai 4, 2020 alitangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama chake binafsi “Birthday Party” na katika uchaguzi huo alipata kura zaidi ya 60,000 kwenye majimbo 12, bado ameonesha nia ya kugombea tena kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2024.