Jumatano , 11th Mei , 2016

Licha ya post mbalimbali mitandaoni zikionyesha ukaribu wa kimahusiano wa Msanii wa Bongo fleva Cyrill a.k.a Kamikaze akiwa na video Queen wake wa katika Video ya 'Shori' Kidoa,Cyril aendelea kuukana uhusiano huo

Msanii wa Bongo fleva Cyrill na video Queen Kidoa

Akizungumza na Enewz Cyril alisema kuwa yeye na video Queen huyo ni washikaji tu, huku kukiwa na fununu kuwa Cyrill alimtosa mwanamke wake wa zamani ili awe na mwananadada huyo.

Ingawa kuna posti zilizopostiwa na kidawa alizoandika ''he is ma real Men'' huku zikiwa zimebebwa na picha za Cyril lakini kamikaze alikanusha kwa kusema kuwa “watu tu wameamua kuichukulia hivyo lakini hakuwa huko”.