Alhamisi , 28th Aug , 2014

Msanii wa muziki Juliani wa nchini Kenya, ameendelea kuonesha moyo wa kujitoa kusaidia wengine, ambapo sasa ametangaza kudhamini michuano ya mpira wa miguu ambao unaendelea huko Dandora maeneo alipokulia.

msanii wa muziki nchini Kenya Juliani

Juliani amesema kuwa mashabiki wa mchezo huu wanaweza pia kumuunga mkono kwa kuchangia vitu kama mipira ama jezi ili kufanikisha mashindano haya.

Hatua ya msanii Juliani imekuwa ni muhimu katika kusaidia vijana wenye vipaji katika soka kujiendeleza na pia kuleta burudani kwa jamii ambayo inaishi huko Dandora.