Jokate Mwegelo
Akiongea ndani ya eNewz Jokate amesema kuna mipango ambayo wanaiweka sawa hivyo mashabiki zake wasubiri kwani tayari ana nyimbo nyingi ambazo ameshazirekodi na akashindwa kuzitoa kutokana na kazi za kampuni yake ya kidoti kuwa nyingi.
Hata hivyo Jokate amesema anategemea kufanya kazi na waongozaji kutoka Kenya na Uganda kwa upande wa bongo movie na hiyo itakuwa siku za karibuni zaidi ikiwezekana mwanzoni mwa mwaka ujao.








