Ijumaa , 2nd Oct , 2015

Star wa Muziki kutoka kundi la WEUSI, Joh Makini ametoa tathmini yake juu ya sababu zinazowafanya wasanii wengi na makundi ya muziki kutokuwa na DJ's rasmi wanaofanya nao shoo, kama ilivyo kwa makundi na wasanii wengi nje ya nchi.

Staa wa Muziki kutoka kundi la WEUSI, Joh Makini

Joh Makini amesema kuwa, kama msanii binafsi amekwishakua na DJ's kadhaa ambao amekuwa akifanya nao kazi na kuwalipa, ingawa zoezi hilo limekuwa gumu kutokana na Ma DJ's hao kutomudu kukaa na kusubiria onyesho kutoka kwa msanii ama kundi moja tu.

Fid Q pia ambaye ni mwana hip hop anayesimama mwenyewe, ametoa tahmini yake juu ya hili, akiugusia mfumo kuwa chanzo cha tatizo hilo.